Discuss with your friends

Would you like to discover for yourself what God is like and how God wants you to live?

Most people like to make these discoveries in a group with their friends. Here are some questions to get your discussion started


    

Discovering Spiritual Community #11

Caring for one another

1. Una shukuru kwa ajili ya nini juma hili?

2. Una sumbukana na nini na jinsi gani tunaweza kukusaidia?

Accountability

3. Ni vipi uliweka kwa matendo tulio jifunza mwisho?

4. Ulishiriki na nani somo lililopita na matokeo yalikuwaje?

5. What needs did you meet in the community last week?

Discover

6. Uliza mtu asome kifungo kimoja kwa wakati.

7. Kuwa na mmoja katika kikundi na aseme kifungo kwa maneno yake mwenyewe.

8. Uliza kikundi kama amewacha au kuongeza kitu.

Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kuba tiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana.Lakini kwa hakika Yesu hakubatiza, wanafunzi wake ndio waliokuwa wakibatiza watu.Bwana alipopata habari hizi aliondoka Yudea akarudi Galilaya.Katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.

Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.Kisima cha Yakobo kilikuwa hapo na kwa kuwa Yesu alikuwa amechoka kutokana na safari, aliketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.”Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”

11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi?12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena.14 Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”

15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuchota maji!”

16 Yesu akamjibu, “Nenda kamwite mumeo, kisha uje naye hapa.”17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwam bia, “Umesema kweli kuwa huna mume.18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!”

19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii.20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu lakini ninyi Way ahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

21 Yesu akamjibu, “Mama, niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu.22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwab udu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi.23 Lakini wakati unakuja, tena umekwisha timia, ambapo wale wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii ndio anaowataka Baba.24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masihi.”

Read full chapter